Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,ameonyesha kutoridhishwa na ujenzi upanuzi Kituo cha Afya Salawe wilayani Shinyanga, huku Milango yake ikiwa imetengenezwa chini ya kiwango.
Macha amefanya ziara hiyo leo Mei 17,2024 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali.
Amesema upanuzi ujenzi wa Kituo hicho cha Afya Salawe umetumia fedha nyingi, lakini hadi sasa haujakamilika kujengwa wala kuanza kutoa huduma za awali kwa wagonjwa, huku Milango ikitengenezwa chini ya kiwango.
"Mradi haupo vizuri hakuna umakni yaani zimetumika shilingi Bilioni 1.2 hakuna kinachoendelea,Mradi kama umetelekezwa, Milango haina ubora, halafu mnasema mnampongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi, acheni ku copy na ku paste mnampongeza Rais kwenye mambo ya hovyo hivi,"amesema Macha.
"Fedha zote hizi ambazo zimetumika kwenye ujenzi wa Kituo hiki cha Afya kingekuwa tayari kimeanza kutoa huduma kwa wananchi,mngetoa kipaumbele kwenye Majengo Muhimu ya OPD,Maabara na Mochwari lakini mmejenga holela bila "Plan"" ameongeza Macha.
Aidha,ameagiza Mafundi ambao wametengeneza Milango pamoja na kupaka rangi kwenye ujenzi wa Kituo hicho, wafike kwa Mkuu wa wilaya kwa hiari yao wenyewe, ili wahojiwe na kufanya Marekebisho haraka.
Amesema kwa sasa hawezi kutoa maamuzi yoyote,bali anatoa Miezi Mitatu ya Tathmini,kwamba hadi kufikia Agosti mwaka huu atarudi tena ili kuona utekelezaji wake, kwa kuanza na umaliziaji wa majengo ya kipaumbele kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,ameonyesha kusikitishwa na kusuasua kukamilika ujenzi wa Kituo hicho,kwamba fedha ambazo zimetumika ni nyingi sana ambazo Kituo kingekuwa kimeanza kufanya kazi, na kutolea Mfano Vituo vya Afya ambavyo vilipewa Sh.milioni 500 vimekamilika na kuanza kutoa huduma.
"Mkuu wa Mkoa Maagizo yako yote ambayo umeyatoa nitayafanyia kazi,tena bahati nzuri ninauzoefu na Miradi ya namna hii, hapa kuna fedha zimechezewa," amesema Mtatiro.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kisena Mabuba, ambaye amekuta Mradi huo ukiwa umeshanza kujengwa, amesema Mikakati ya Halmashuri ambayo wameweka ili kukamilisha Majengo Muhimu ya kuanza kutoa huduma, wameshatenga Sh.milioni 50 ambazo watazitoa Mwezi huu.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akisoma taarifa ya ujenzi wa upanuzi wa Kituo hicho cha Afya Salawe, amesema ulianza mwaka (2021/2022) na fedha iliyotumika ni Sh.bilioni 1.2 na bado hakijaanza kutoa huduma na fedha imekwisha.
Ametaja Mikakati ya Halmashauri ili kukamilisha ujenzi na kuanza kutoa huduma za Matibabu,kwamba katika mwaka wa fedha (2023-2024) wametenga Sh.milioni 25 kupitia mapato ya ndani,na mwaka wa fedha (2024-2025) wametenga tena Sh.milioni 15.
Ametaja faida ya Kituo hicho cha Afya Salawe kitakapokamilika kujengwa kwa upanuzi wake, kwamba kitapunguza Vifo vya Mama na Mtoto,kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma za Matibabu.
Nao baadhi ya wananchi wa Salawe, ameiomba Serikali kukamilisha haraka upanuzi wa Kituo hicho, ili wapate huduma bora za matibabu karibu na kunusuru Afya zao.
Ziara ikiendelea Kituo cha Afya Salawe.
Ziara ikiendelea Kituo cha Afya Salawe.
Ziara ikiendelea Kituo cha Afya Salawe.
Ziara ikiendelea Kituo cha Afya Salawe.
Ziara ikiendelea Kituo cha Afya Salawe.
Social Plugin