Na Sumai Salum _Kishapu
Timu ya Ngundangali Fc imeichapa Madrid Fc ya Mwanulu bao 1-0 goli lililofungwa na Bakari Said mshambuliaji namba tisa(9) katika kipindi cha kwanza dakika ya 42 Ligi ya Shagy Cup inayoendelea Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mchezo huo umerindima leo Mei 7,2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Lubaga wilayani humo uliozinduliwa rasmi na Mbunge wa jimbo la Kishapu na mdhamini wa Ligi hiyo Mhe. Boniphace Butondo mnamo Mei 4,2024.
Mwamuzi wa mchezo huo Tungu Said ametoa kadi za njano tatu (3) kwa Bakari Said,Mau Hassan na Boban wachezaji wa Ngundangali Fc,kadi moja ya njano kwa Masunga Paul mchezaji wa Madrid huku kadi nyekundu ikielekezwa kwa Mathias Emmanuel mchezaji wa Madrid Fc.
Aidha, hapo jana Mei,6,2024 mchezo ulikuwa kati Bodaboda Fc dhidi ya Farmer Fc ambapo walitoka sare ya 0-0 na mchezo huo utarudiwa Mei 18,2024 katika viwanja hivyo hivyo.
Shagy Cup inayochezwa na timu 16 kutoka ndani na nje ya Jimbo la Kishapu imelenga kukuza vipaji vya wachezaji,kutoa ajira kwa vijana pamoja na kujenga umoja na mshikamano kwa jamii ya wana Kishapu.
Kikosi cha Madrid Fc ya Mwanulu dhidi ya Ngundangali Fc leo Mei,7,2024 katika viwanja vya Shule ya msingi Lubaga ligi ya Shagy Cup wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Social Plugin