Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanikiwa kutekeleza vipaumbele vitano katika mwaka wa fedha 2023/24 ambavyo ni pamoja na kukamilisha Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na Mitaala ya Elimu na kuanza utekelezaji wake kwa lengo la kuimarisha ujuzi kwa wahitimu.
Akitaja vipaumbele hivyo bungeni Dodoma leo, Prof Adolf Mkenda amesema wamefanikiwa kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa mafunzo ya amali kwa sekondari na vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, kuwezesha Ongezeko la fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu.
Vipaumbele vingine kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuimarisha uwezo wa nchi katika tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Social Plugin