Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BARRICK ILIVYOADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Mfanyakazi bora wa Barrick, Dativa Katabaro, akipokea zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Philip Mpango.
Wafanyakazi wa mgodi wa Barrick waliochaguliwa wafanyakazi bora wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Anamringi Macha.

Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakishiriki katika maandamano ya Mei Mosi.
Wafanyakazi waliotunukiwa vyeti katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu walijumuika na wafanyakazi wenzao kutoka taasisi mbalimbali katika maadhimisho hayo

 ***

Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini kupitia migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara, iliungana na wafanyakazi wote duniani kuadhimisha siku ya Mei Mosi ambapo wafanyakazi wake walishiriki katika maadhimisho yaliyofanyika katika mikoa ya Arusha,Mara na Shinyanga. 

Mkoani Arusha ambapo sherehe hizo zilifanyika kitaifa,mfanyakazi bora wa Barrick Dativa Katabaro ni miongoni mwa wafanyakazi waliotunukiwa vyeti na zawadi na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Mkoani Shinyanga mgodi wa Barrick Bulyanhulu umewapatia vyeti pamoja na fedha taslimu wafanyakazi waliofanya vizuri katika sekta zao wakati shughuli za uzalishaji zikiendelea katika mgodi huo.

Kampuni ya Barrick imekuwa na utaratibu wa kutoa motisha za zawadi kwa wafanyakazi wake na kuthamini mchango wao kwenye kampuni.

Awali akizungumza mbele ya wafanyakazi na wadau mbalimbali Mgeni rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, aliipongeza kampuni ya Barrick ,kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu unaopatikana Mkoani kwake kwa kuthamini wafanyakazi wake pamoja na kujali maslahi yao pamoja na kuendelea kushirikiana vyema na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com