Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya akizungumza mara baada ya kuzindua mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Mwakilishi wa Balozi wa Uswis nchini Rashid Mbaramula akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Naibu
Meya wa Jiji la Tanga Rehema Mhina akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa mradi
wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na
na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na
kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi
Makorora Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mradi
wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na
na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na
kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchiniNa Oscar Assenga, Tanga
ASILIMIA zaidi ya 90 ya wanafunzi katika shule za Msingi Makorora na Azimio jijini Tanga wapo kwenye hatari kubwa ya kugongwa na pikipiki,magari na vyombo vyengine vya moto.
Hatua hiyo imelilazimu Shirika la Amend Tanzania kutekeleza mradi wa uwekeji wa miundombinu salama ya barabara katika shule hizo ili kuwaepusha na ajali wanazoweza kukumbana nazo.
Akizungumza leo katika uzinduzi wa mradi wa miundombinu salama ya barabaraani katika Shule ya Msingi Makorora na Azimio jijini Tanga, Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimon Kalolo wakati wa uzinduzi wa Miundombinu salama ya barabarani katika shule za Msingi Makorora na Azimio Jijini Tanga .
Alisema wameamua kutekeleza mradi huo kunatokana na wanafunzi hao kutembea kwenda na kurudi shuleni kila siku hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kugongwa na pikipiki, magari na vyombo vingine vya moto.
“Takribani wanafunzi wasiopungua 8 katika shule hizi mbili wamejeruhiwa katika ajali za barabarani katika muda wa miezi 12 iliyopita zote zikihusisha pikipiki”Alisema
Alisema baada ya kushauriana na wadau wa shule hizo wakiwemo wanafunzi na walimu, wanajamii, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Jeshi la Polisi Amend kupitia msaada kutoka kwa Ubalozi wa Uswisi na washirika wake wa serikali.
Alisema baada ya kushauriana wameweka miundombinu salama kwa lengo la kuzuia ajali za barabarani ikiwemo njia za waenda kwa miguu, matuta, vivuko vya pundamilia, alama za barabarani, na elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wote.
“Tumezindua miundombinu mipya ya kuokoa maisha ya watembea kwa miguu hasa watoto katika Shule za Msingi Makorora na Azimio”Alisema
Aliongeza kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watoto wanaotembea kwa miguu ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari kubwa ya kupata majeraha ya barabarani nchini Tanzania.
“Tofauti na watoto katika nchi zilizoendelea wengi wa watoto wa shule katika maeneo ya mijini mkoani Tanga, na Tanzania kwa ujumla, wanatembea kwenda shule bila kusindikizwa na mtu mzima”Alisema
Alisema pia kwa Bara la Afrika watoto wako katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ikilinganishwa na eneo lingine lolote duniani.
“Kwa bahati nzuri njia za kuzuia ajali hizi zinaeleweka vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaepusha watoto na msongamano wa magari na kupunguza mwendo kasi wa magari katika maeneo ambayo watoto wanavuka barabara”Alisema
“Mradi huu unaungwa mkono na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na una bajeti ya shilingi za Kitanzania 424,983,396 (takriban Faranga za Uswisi 150,000)”Alisema
Aliongeza mradi huo ulianza Septemba mwaka 2023 ambapo shughuli nyingine za mradi zimejumuisha mafunzo ya waendesha pikipiki (bodaboda) 300 ndani ya Jiji la Tanga, waendesha pikipiki 253 mkoani Dodoma ikiwemo kampeni ya uhamasishaji kuhusu masuala ya usalama wa pikipiki, na kuanzishwa kwa 'Kanuni za Maadili' kwa waendesha pikipiki 200 zaidi watapewa mafunzo jijini Tanga ifikapo Juni 2024.”
Mwisho
Social Plugin