Wameazimia hayo leo
Mei 10, 2024, wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kujadili ajenda
mbalimbali amoja nakupokea taarifa kutoka taasisi mbalimbali.
Wametoa kauli hiyo kutokana na kero ya muda mrefu hiyo kuwa ya muda mrefu hasa kwa kata Didia tangu mwaka 2022 ankara za maji kuwa na bei kubwa ukilinganisha na maeneo mengine ya halmshauri hivyo kutoa kauli ya pamoja ya kutokudumiwa na Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).
Akiwasilisha kero wakati
wa kikao hicho Diwani wa kata ya Didia Richard Masele amesmea amelalamikia bei
kubwa ya maji wanayotozwa wananchi wa kata ya Didia licha ya suala hilo
kupatiwa ufumbuzi na mkuu wa wilaya lakini bado haijabadilishwa.
“Wakati tunahamishwa
kutoka RUWASA kwenda SHUWASA binafsi sikukubaliana na suala lile kwasababu sikuwa
na uhakika kuwa tutakwenda kunufaika na ndio yanayojitokeza sasa kijiji cha
Mwanono na Mwamalulu kwenye kata ya Didia havina maji, mimi maendekezo yangu nani maombi
ya wananchi kwa niaba ya wananchi kama wameshindwa kutuhudumia waturudishe kule
tuliokuwa tuliokuwa RUWASA hatukuwa na malalamiko haya”, amesema Diwani Masele.
“Mheshimiwa mkuu wa
wilaya alizungumza na mkurugenzi wa EWURA na kukubaliana kuwa bei hiyo ibadilishwe
lakini mpaka leo hakuna mabadiliko yeyote juu ya bei hizo nikuombe mheshimiwa
mwenyekiti kupitia baraza hili tupate azimio la pamoja juu ya suala hili”, ameongeza
Diwani Masele.
Diwani wa Kata ya
Iselamagazi Isack Sengerema amekiri kupokea taarifa kutoka Mamalaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) juu ya kupanda kwa bei ya maji
kwenye kata yake kutoka Sh. 1,000/= hadi Sh. 2,550/=.
“Jambo hili ni gumu sana kwa sababu maji ni huduma lakini SHUWASA wamefanya kuwa biashara haiwezekani bei ya maji ilingane sawa na bei ya Petrol ambayo yanasafirishwa kutoka nje ya nchi, hata mimi nimepokea taarifa ya kupanda kwa maji kutoka Sh. 1,000/= hadi Sh. 2,550/=.yani sis indo tunakwenda kulipa bei kubwa kuliko sehemu zote.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboji amesema kutokana
na malalamiko yaliyotolewa na madiwani juu ya bei kubwa ya maji kwenye baadhi
ya maeneo ndani ya halmashauri hiyo ameiomba ofisi ya mkuu wa wilaya Shinyanga Mamalaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) isitishe kutoa huduma
kwa wananchi waishio vijijini amoja na kutoa kauli ya baraza juu ya suala hilo.
“Nikuombe ofisi ya mkuu wa Wilaya pamoja na mazungumzo yako mazuri na wizara Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) hawatakiwi kuhudumia maeneo ya vijijini kwasababu ya kero inayoonekana, Sh 2,550/= kwa maisha ya mwananchi wa kawaida anaeishi kwenye nyumba ya nyasi hawezi kumudu gharama hizi, sisi kama baraza tunaiomba ofisi ya mkuu wa wilaya iwaondoshe Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) wabaki maeneo ya mjini sehemu zilizo na mzunguko wa fedha lakini kwetu sisi kama baraza la madiwani hili ni azimio kuwa hatuwahitaji” , amesema Ngasa Mboji.
Akitoa ufafanuzi juu
ya suala hilo mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambaye ni kaimu meneja kanda ya Iselamagazi
Martini Shemgaa amesema zipo taratibu za upangaji wa bei kulingana na maeneo
husika na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo ili kuendeea kutoa huduma kwa
wateja wao.
Awali akisoma taarifa
ya robo tatu ya mwaka 2023/2024 kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sitewart
Makali mbali na masuala mbalimbali yakimaendeleo ia amebainisha uwepo wa mliuko
wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo watu wawili wamepoteza maisha kutokana na
ugonjwa huo.
"Halmashauri yetu imeokea taarifa ya uweo wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo tarehe 30/04/2024 jumla ya watu 11 waligundulika kuambukizwa ugojwa huo katika kata ya Mwakitolyo, ambapo watu wawili walifariki wengine 9 walipatiwa matibabu na kuruhusiwa", amesema Sitewart Makali.
‘Kufuatia mlipuko huo halmashauri
imechukuwa hatua za kukabiliana na ugonjwa huo kwa kugawa dawa za kutibu maji
kwa kaya 462, kutibu visima vya maji 16 na kutoa elimu kwa jamii jinsi ya
kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu’, ameongeza Sitewart Makali.
Social Plugin