Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wameungana na wafanyakazi wengine Duniani kushiriki katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambayo kitaifa yamefanyika Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Maadhimisho haya yamepambwa na kauli mbiu isemayo "Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha".
Pia vituo vingine vilivyoshiriki maadhimisho hayo ni Dar es Salaam, Mwanza,Iringa,Mtwara, Bukoba, Songea, Zanzibar (Unguja na Pemba), Tabora, Kigoma, Songwe na Tanga
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakipita mbele ya Jukwaa Kuu huku wakiwa na bango lenye ujumbe kuhusiana Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapungia mkono Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wakipita mbele ya Jukwaa Kuu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya Kuingia katika uwanja wa Uhuru uliopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yalifanyika.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dar es Salaam wakipita mbele ya Jukwaa Kuu huku wakiwa na bango lenye ujumbe kuhusiana Wafanyakazi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru uliopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru uliopo katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Zanzibar wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Social Plugin