KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,akisisitiza jambo wakati akifungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,akizungumza wakati akifungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
Kaimu Msajili wa Baraza la ushindani (FCT) Be.Kunda Mkenda,akizungumza wakati wa semina ya baraza hilo kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma yenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Uchumi FCT, Kulwa Msogoti ,akizungumza wakati wa semina ya baraza hilo kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma yenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,(hayupo pichani) wakati akifungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
Ofisa Sheria Mkuu Hafsa Said,akichangia mada wakati wa semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
WADAU mbalimbali wakichangia mada wakati wa semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
BARAZA la ushindani (FCT) limetoa elimu kwa wadau mkoani Dodoma yenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji.
Akifungua semina hiyo jijini Dodoma Mei 9, 2024, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Kaspar Mmuya, amepongeza baraza hiyo kwa kutoa elimu hiyo itakayowasaidia watanzania kwenye biashara zao kwa kuongeza kasi ya uwajibikaji ili kujiepusha na migogoro ya kiushindani.
“Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuunda chombo hichi na Rais Samia Suluhu Hassan ametoa nafasi kupitia FCT kutoa maoni ili kudhibiti soko na ushindani na kuleta usawa,”amesema.
Awali, Kaimu Msajili wa Baraza hilo, Kunda Mkenda amesema elimu inayotolewa na FCT ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kisheria kwa kuwa ni chombo cha rufaa kilichoanzishwa chini ya kifungu cha 83(1) cha Sheria ya Ushindani namba nane ya Mwaka 2003.
Kwa upande wao, Mkuu wa Idara ya Uchumi FCT, Kulwa Msogoti na Ofisa Sheria Mkuu Hafsa Said, wameeleza namna baraza linavyoendesha mashauri yake na kwamba kwa kipindi cha Mwaka 2007 hadi Machi, 2024, mashauri 443 yalisajiliwa kati ya hayo 429 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi huku 13 yakiwa kwenye hatua mbalimbali za usikilizwaji.
Aidha, washiriki wa semina hiyo, Faustine Mwakalinga na Grace Onea, wamepongeza baraza kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi kuwa mabalozi kwenye maeneo yao ili kuepuka migogoro ya kiushindani.
Social Plugin