Ikiwa imepita siku moja tangu Bunge kuidhinisha matumizi ya ya Shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya Wizara ya Kilimo katika mwaka 2024/2025 kwa ajili ya utekelezaji wa mipango nchini, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amesema Wananchi wa Mkoa huo wamepokea kwa matumaini makubwa sana namna ambavyo Wizara inafanya kazi kuhihisha huduma zinawafikia wakulima.
Akizungmza katika kipindi cha Sentro kinachoruka Clouds TV, Mhe. Mtaka amesema Mkoa wa Njombe umenufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara hiyo kuanzia kwenye upatikanaji wa mbegu bora, mbolea ya ruzuku pamoja na ukarabati wa miundombinu ya umwagilaiji.
Pia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuipa nguvu Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua na kuhifadhi mazao ya wakulima kwani mkoa huo ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mazao katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.
Kwa upande mwingine, RC Mtaka amesema kuwa kwa miaka 60 ya Uhuru, Bashe ndio Waziri aliyefanikiwa zaidi kuleta mapinduzi ya Kilimo kwa vitendo.