Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe alipata nafasi ya kupita katika maonesho ya Kilimo yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma baada ya kuwasilisha Bajeti ya Kilimo, jana Mei 02, 2024.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya 'FROM LAB TO FARM 2024' yamelenga kuonesha jinsi ubunifu na teknolojia za kisasa zinavyoweza kuchochea maendeleo kwenye Sekta ya Kilimo.
Bashe aliongozana na wageni mbalimbali waliofika Bungeni hapo wakiwemo baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi, wadau wa Kilimo bila kumsahau Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Ndg. Abdulmajid Nsekela kwajili ya kusikiliza mipango ya serikali katika kukiendeleza Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
Social Plugin