Watu 11 wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari Cha Mtibwa mkoani Morogoro wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia Hitilafu ya umeme Kiwandani hapo .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama ameiambia Matukio Daima media kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa saba na nusu, usiku wa kuamkia leo.
SACP Mkama amesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye mtambo wa kupitisha mvuke wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.
Kamanda huyo wa Polisi amesema waliofariki dunia ni pamoja na raia wa kigeni wa nchi tatu tofauti na ambao ni wataalamu wa umeme na mitambo waliokuwa kwenye chumba cha kuendesha mitambo hiyo.
Aidha majeruhi watatu wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali ya Misheni ya Bwagala kwa ajili ya matibabu zaidi.
CHANZO - MATUKIO DAIMA
Social Plugin