Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wakili Stephen Byabato leo amemkaribisha Mhe. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Mahamat amewasili nchini kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Sherehe za miaka 20 ya kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yatakayofanyika tarehe 25 Mei 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi pamoja na Wageni zaidi ya 120 kutoka ndani na nje ya Tanzania. Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Social Plugin