SERIKALI KUJENGA SHULE 100 MPYA ZA AMALI


Waziri wa Elimu, Prof Adolf Mkenda amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na sekondari za amali ili kuongeza fursa za mafunzo kwa kuwezesha ujenzi wa shule mpya za sekondari za amali 100 ambapo kati ya hizo shule 26 zitaanza kupokea wanafunzi kuanzia Januari 2025.


Aidha, Prof. Mkenda amesema ujenzi wa shule za amali utapewa kipaumbele katika maeneo ambayo hayana vyuo ya mafunzo ya ufundi stadi.


Kwa upande mwingine, Waziri huyo wa Elimu amesema serikali itaendelea na ujenzi wa vyuo 65 vya mafunzo ya ufundi stadi, kati ya hivyo 64 ni vya wilaya na kimoja ni cha ngazi ya Mkoa wa Songwe.


Vilevile, Serikali imeongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo 29 vilivyokamilisha ujenzi na
 itaendelea na ujenzi wa miundombinu ya nyongeza katika vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi kama vile Ndolage-Muleba, Ileje, Newala, Ngorongoro, Gorowa - Babati, Urambo, Kasulu, Mabalanga - Kilindi, Nkasi na Kanadi - Bariadi, ili kuviwezesha vyuo hivyo kufikia viwango vya msingi vya utoaji wa mafunzo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post