Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Simon Mnkondya maarufu Mr Manguruwe amekuja na kali ya kugawa tiketi bure kwa mashabiki wa soka Mkoani Arusha wapate burudani kwenye mechi ya leo kati ya Simba SC na KMC katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Wakati Mr. Manguruwe akigawa tiketi kwa mashabiki wa Simba SC washabiki wa soka huku wakiibua shangwe na kupiga kelele wakimwita Mr. Manguruwe! Mr. Manguruwe Mr. Manguruwe!! Mr. Manguruweeeeeee!!.
Mr. Manguruwe pia ametangaza kuja na mashindano ya kubeba nguruwe wakubwa wa Zamahero Dodoma na kumkaribisha Mwarabu Faita, Keyoyo , Komando Madafu na Mandonga kuja kujaribu bahati yao ya kubeba nguruwe na endapo mshindani ataweza kubeba nguruwe dume atapata kitita cha milioni 50 sawa na dola 23,000 za Kimarekani.
Wasiliana na M.r Manguruwe 0763755755 na 0767600300.
Social Plugin