"Katika kuimarisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu, Serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya TEHAMA na teknolojia nyingine za kufundishia na kujifunzia kwa lengo kuongeza ufanisi katika ufundishaji;
imeendelea kusimamia bunifu mbalimbali zilizobuniwa kupitia watumishi na wanafunzi ili ziweze kufika hatua ya kuuzika sokoni, bunifu hizo ni uundaji wa mita za malipo kabla ya matumizi; Programu ya Bi - Shamba na Programu ya Leo Leo Gulio” - Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia