Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Carolyne Nombo wakijadiliana jambo na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Shaban Hamis Taletale katika viwanja vya Bunge leo Mei 08, 2024.
Prof. Mkenda aliwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni, Jana Mei 07, 2024 akiliomba Bunge kuidhinisha zaidi ya Shilingi Trilioni 1.9 zitakazoelekezwa kwenye vipaumbele vitano vinavyolenga kuleta mageuzi ya Elimu nchini huku msukumo mkubwa ukiwekwa kwenye Elimu ya ujuzi ili kuwawezesha wahitimu katika ngazi mbalimbali kujiajiri na kuajiri wengine.
#TunaboreshaElimuYetu
#ElimuUjuziNdioMwelekeoWetu
Social Plugin