Waendesha Baiskeli Mabingwa wa Kanda ya Ziwa mapacha Kulwa Mahega na Dotto Mahega wamefariki dunia kwa ajali kwa kugongwa na gari aina ya Land Cruiser wakiwa kwenye pikipiki eneo la Ndala Manispaa ya Shinyanga leo mchana Alhamisi Mei 9,2024.
Mwenyekiti wa Chama cha Wapanda Baiskeli Mkoa wa Shinyanga Kashi Salula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
"Tumepokea taarifa za kifo cha vijana wetu kwa masikitiko makubwa, wamefariki dunia kwa kugongwa na gari wakiwa watatu kwenye pikipiki. Inasikitisha sana watu waliozaliwa siku moja, wakafa siku moja, ...tulikuwa tunawaandaa kwenda kushiriki mashindano nje ya nchi",amesema Kashi.
SALAMU ZA RAMBI RAMBI
"Mkurugenzi wa CM Entertainment Na Muandaaji wa mashindano ya Mbio za Basikeli mkoani Shinyanga Ambazo hufanyika katika Sherehe za Wakulima Maarufu NaneNane anatoa Salamu za Pole kwa Familia,Ndugu,Jamaa na Tasnia ya Waendesha baiskeli kwa Msiba huu mzito wa waliokuwa washindi wa mbio za baiskeli mwaka 2023 KULWA na DOTO MAHEGA na kuendelea kuwambea Uvumilivu katika kipindi Hiki Kigumu hakika BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE AMEN!!!"🙏🏻
#TutaOnanaBaadae🕯️
Social Plugin