MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camilius Wambura amemvisha Nishani ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
RPC Magomi ni mmoja kati ya Maafisa wa Polisi 26 wa ngazi mbalimbali kutokea Kanda tano (5) inayojumuisha Mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Katavi, Tabora na Singida.
Sherehe hizi za uwasilishaji Nishani zimefanyika leo tarehe 25 Mei, 2025 katika Viwanja vya FFU vilivyopo Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora.
Social Plugin