Timu ya Viongozi kutoka Bodi ya Nyama Tanzania wakiongozwa na Kaimu Msajili Mkuu John Chasama wamefika katika Mradi wa Kijiji Cha Nguruwe Dodoma kinachomilikiwa na Mr. Manguruwe na kubaini baadhi ya mapungufu kama vile kuwa na Nguruwe wengi sana kuliko leseni yake na ukosefu wa karo la dawa ya kudhibiti magonjwa.
Kwa upande mwingine, wamemtaka mdau wao huyo kuweza kufanyia kazi changamoto hizo na kukata leseni mpya inayoruhusu Mifugo mingi zaidi kwani kwa sasa leseni yake inaruhusu Mifugo 49 tu.
Naye, Mr. Manguruwe ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji Cha Nguruwe Project kilichopo Bahi Mkoani Dodoma amesema wakati wanakuja kwenye mradi wake huo hakuwa na taarifa na hakuwepo ila amepata ujumbe wao kupitia Mitandao na ameahidi kufanyia kazi ushauri wao haraka iwezekanavyo ili kuzidi kukuza sekta ya kilimo na uwekezaji nchini.
Social Plugin