WAFANYAKAZI DIT WASHAURIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA MARA KWA MARA

Wafanyakazi na wanafunzi wa DIT kampasi ya Mwanza wameshauriwa kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujua kama wanaviashiria vya magonjwa yasiyoambukiza ili wapatiwe matibabu ya mapema.

Ushauri huu umetolewa leo katika Tamasha la afya day lililoandaliwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT kampasi ya Mwanza na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali  waliojitokeza kushiriki na kupima afya zao.

Mganga mkuu wa Jiji la Mwanza Dr Sebastian Pima akimwakilisha mganga mkuu wa  mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amewaomba wananchi kuzingatia suala la afya kwa kufanya mazoezi pamoja na kula mlo kamili.

Mwakilisha wa mkurugenzi wa DIT Bwn, William Lohay amesema Tamasha la afya day ni utekelezaji wa mwongozo wa Serikali wa kuhakikisha afya za wafanyakazi zinakuwa imara.

Wataalam wa magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya rufaa ya kanda Bugando wametoa huduma mbalimbali ikiwemo vipimo na ushauri wa namna ya ulaji Bora na kuzingatia mazoezi ili kujiepusha na maradhi na gharama ambazo zinaweza kujitokeza.

Baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu wameishukuru Taasisi ya DIT kampasi ya Mwanza kuwasogezea huduma za vipimo bure.

Awali Tamasha hilo lilianza kwa matembezi ya kilomita 6 yakiwajumuisha wafanyakazi na wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali na Shule za sekondari zilizopo Mwanza.

Tamasha hilo lenye lengo la kuboresha afya za wafanyakazi na wanafunzi limepambwa kwa michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mbio za magunia, Mpira wa miguu,mpira wa Pete,kufukuza kuku,kuruka kamba na michezo mingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post