Mha. Nicholaus Kayombo akiwaeleza wanafunzi wa VETA Kihonda kuhusu utaratibu wa kuomba leseni za ufungaji umeme kupitia mfumo wa LOIS wakati wa semina kwa wanafunzi hao iliyofanyika chuoni hapo.
.........
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Kanda ya Kati, imetoa elimu kwa wanafunzi zaidi ya 500 wa Vyuo vya Ufundi Stadi vya Kongwa, Kihonda na Mikumi kuhusu utaratibu wa kuomba leseni za ufungaji mifumo ya umeme kwa lengo la kuhakikisha usalama, ubora wa huduma na utekelezaji wa matakwa ya sheria.
Mafunzo hayo yaliyohitimishwa leo 22 Mei 2024, yalianza tarehe 20 Mei 2024, na kujumuisha wanafunzi 76 wa fani ya umeme wa chuo cha VETA Kongwa, 98 wa fani hiyo hiyo wa VETA Mikumi na 304 wa VETA Kihonda, 131 kati ya hao wakiwa wa fani ya umeme.
Mhandisi wa Umeme Mwandamizi kutoka EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo ameeleza kuwa, leseni za ufungaji mifumo ya umeme hutolewa kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131 inayomtaka yeyote anayefanya shughuli za ufungaji mifumo ya umeme nchini kuwa na leseni ya EWURA.
“Ni muhimu wote kutambua kwamba suala la kuwa na leseni ni takwa la kisheria hivyo ni lazima kuwa na leseni ili kutambulika na kuafanya kazi stahiki inayoendana na ngazi ya elimu husika” alieleza.
Maombi ya leseni za ufungaji umeme hufanyika mtandaoni kwenye mfumo wa LOIS, uliopo katika tovuti ya EWURA www.ewura.go.tz, mwombaji anapaswa kuwa na cheti cha mafunzo, picha ya pasipoti, kitambulisho (kura, NIDA au leseni ya udereva) na wasifu (CV).
EWURA imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wadau wake ili kuimarisha uelewa wa masuala mtambuka kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji ikiwamo kupokea malalamiko na kutatua migogoro inayotokana na huduma zinazodhibitiwa.
Mha. Nicholaus Kayombo akiwaeleza wanafunzi wa VETA Kihonda kuhusu utaratibu wa kuomba leseni za ufungaji umeme kupitia mfumo wa LOIS wakati wa semina kwa wanafunzi hao iliyofanyika chuoni hapo.
Wanafunzi wa fani ya umeme ngazi ya kwanza wa chuo cha VETA Mikumi wakiendelea na mafunzo yalitotolewa na EWURA chuoni hapo kuhusu utaratibu wa kuomba leseni za ufungaji umeme
Baadhi ya Wanafunzi wa VETA Kongwa, wanaosoma fani ya umeme wakisikiliza maelezo ya namna ya kupata leseni za ufungaji umeme kutoka EWURA wakati wa mafunzo yaliyofanywa na EWURA chuoni hapo.
Social Plugin