ILANI YA CCM 2020/2025 YATEKELEZEKA KWA 91.08% KISHAPU.. SULEIMAN NCHAMBI ATIA NENO

 Na Sumai Salum - Kishapu 

Ilani ya Chama  Cha Mapinduzi CCM 2020/2025 Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga imetekelezwa kwa asiliamia 91.08% katika idara mbalimbali.

Akisoma taarifa ya kata ya utekelezaji ilani hiyo  leo Mei 27,2024 kwenye Mkutano mkuu wa CCM  uliofanyika katika ukumbi wa SHIRECU  Diwani wa Kata hiyo Mhe.Joel Ndettoson amesema kuwa ushirikiano wa wananchi na wataalamu wa kata na Halmashauri umefanikisha utekelezaji huo.

Aidha taarifa hiyo imebainisha kukamilika kwa baadhi ya  miradi  huku mingine ikiwa  katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ikiwemo idara ya Elimu,Afya na mazingira,Maji,Tanesco,Miundombinu (barabara),Taarifa ya Hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, kituo cha afya Kishapu na Zahanati ya Lubaga,Kilimo na Mifugo,Mwenendo wa wafanyabiashara na viwanda pamoja na Polisi Jamii.

"Baadhi ya maeneo wananchi wake wamesaidia kuanzisha miradi mbalimbali hasa wa elimu ikiwemo shule ta sekondari Isoso iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na baadaye tukapata fedha kutoka serikali kuu na kukamilisha na hadi sasa  imepelekwa kata yetu kuwa na jumla ya Sekondari mbili na shule za msingi saba", amesema Ndettoson wakati akisoma taarifa ya kata ya utekelezwaji ilani hiyo.

Hata hivyo kutokana na taarifa hiyo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo Bw. Fabian Makongo na Bi. Janeth Philipo wamemuomba Diwani kuendelea kusimamia kwa bidii utekelezaji miradi hasa miundombinu na upatikanaji huduma bora kwenye idara ya afya huku diwani akiwasihi ukataji wa bima za afya ili kupunguza gharama za matibabu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe. Suleiman Nchambi amempongeza Diwani wa kata hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na kuwa kiongozi wa mfano ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwasihi wanaCcm kuendelea kuwa wamoja, kupendana,kuhurumiana na kuhudumiana.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude amewapongeza viongozi na wanachama hao kwa umoja na mshikamano wanaliona huku akiwasihi wanapoendea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 kuchagua viongozi Bora ambao watamsaidia kuwatumikia wananchi.

Diwani wa Kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Joel Ndettosn akisoma taarifa ya kata ya utekelezaji wa ilani ya Ccm 2020/2024 iliyotekelezeka kwa 91.08% katika idara kumi na mbili (12) leo Mei 27,2024 katika ukumbi wa Shirecu Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Kishapu kwenye mkutano mkuu wa usomaji taarifa ya kata ya utekelezaji ilani ya Chama hicho Leo Mei,27,2024 uliofanyika katika ukumbi wa SHIRECU.
Mjumbe wa mkutano mkuu taifa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Nchambi akizungumza kwenye mkutano mkuu wa usomaji taarifa ya utekelezaji ilani ya Ccm Kata ya Kishapu Leo mei 27,2014 katika ukumbi wa SHIRECU Wilayani humo.
Mwenyekiti wa Ccm kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga ,Paul Shagembe
Katibu wa CCM kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Cornel Zengo akizungumza kwenye mkutano mkuu wa usomaji taarifa ya kata ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho Leo Mei 27,2024 

Viongozi wa dini ya kiislamu na Kristo wakifanya maombi kwenye mkutano mkuu wa usomaji taarifa ya Kata ya utekelezaji ilani ya Ccm kata ya Kishapu Mwaka 2020/2024 uliofanyika Mei,27,2014 katika ukumbi wa SHIRECU wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Kikundi cha ngoma kutoka Mwabusiga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakitumbuiza katika mkutano mkuu wa usomaji taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kata  ya Kishapu
Wajumbe wa mkutano mkuu,sekretarieti ya chama,viongozi wa dini,wazee maalufu,wataalamu na viongozi mbalimbali akiwa kwenye mkutano mkuu wa usomaji taarifa ya utekelezaji ilani ya Ccm Kata ya Kishapu Mkoani Shinyanga Leo Mei,27,2024 katika ukumbi wa SHIRECU.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post