Na Zena Mohamed,Dodoma
JESHI la kujenga Taifa (JKT)limewaita Vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha sita kwa Mwaka 2024 kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa Mwaka 2024.
Wito huo umetolea Jijini hapa leo,Mei 24,2024 na Mkuu wa Utawala Tawi la JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu wito huo ambao umewataka vijana hao kuripoti makambini kuanzia Juni mosi hadi Juni 7,2024.
Brigedia Jenerali Mabena amesema vijana hao wamepangia katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara,JKT Msange-Tabora,JKT Ruvu-Pwani,JKT Mpwapwa,Makutupora JKT-Dodoma,JKT Mafinga-Iringa,JKT Mlale-Ruvuma,JKT mgambo na JKT Maramba-Tanga
Nyingine ni JKT Makuyuni-Arusha,JKT Bulombora,JKT Kanembwa na JKT Mtabila-Kigoma,JKT Itaka-Songwe,JKT Luwa na JKT Milundikwa-Rukwa,JKT Nachingwea-Lindi,JKT Kibiti-Pwani na Oljoro JKT-Arusha.
"JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa ambavyo watavipata na orodha kamili ya majina ya Vijana hao na Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo ya makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz,"amesema Brigedia Jenerali
Hata hivyo JKT limeonya baadhi ya watu wasiowaaminifu kuacha vitendo vya kitapeli kwani mafunzo hayo yanatolewa bure na vifaa vyote vinavyohitajika vimewekwa kwenye tovuti tayari.
Pamoja na hayo ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani imeendelea kuboresha makambi na vijana wote watakao wasili hakutokuwa na changamoto yoyote.
Vilevile ametaja faida ya mafunzo hayo kuwa licha ya kufundishwa uzalendo na Ukakamavu lakini pia katika kambi hizo kunakuwepo na mafunzo ya ujasiriamali kama vile kilimo, Ufugaji, Uvuvi na namna ya kutengeneza sabauni za maji na vipande bila kusahau sabauni za usafi majumbani.
" Mafunzo haya yamekuja baada ya kuona sio wote wanaishia kuwa wanajeshi au waajiriwa hivyo wengine waweze kutoka na ujuzi uwasaidie huko watakapokwenda,"amesema
Social Plugin