Nyumba ya Bi Catherine Atanael
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa akizungumza na Wananchi walioathiriwa na mafuriko
Na Mariam Kagenda - Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwassa amemuahidi kumpatia kiwanja na kumjengea nyumba bi. Catherine Athanael miaka 60 ambaye nyumba yake imedondoshwa na mafuriko katika mtaa wa Migera manispaa ya Bukoba na huku akiwa na jukumu la kuwalea wajukuu zake sita ambao ametelekezewa na watoto wake.
Mwassa ametoa kauli hiyo wakati akikagua nyumba ambazo zimeathirika na mafuriko ya mvua katika manispaa ya Bukoba.
Amesema kuwa ofisi yake imeguswa na maisha anayoishi mjane huyo na hivyo amehaidi kumpatia kiwanja na kumjengea nyumba ya vyumba viwili ili aweze kupata mahali pa kujiifadhi na ametumia nafasi hiyo kuwataka watoto wa bibi huyo kurudi nyumbani ili waweze kulea watoto wao na kuwa serikali iko tayari kuwapatia mitaji ili wafanye biashara na kuweza kuwatunza watoto wao.
Kwa upande wake bi. Catherine Athanael amesema kwa sasa hana pa kuishi na amehifadhiwa na msamaria mwema pamoja na hao wajukuu wake na hajui hatima ya maisha yake kwani afya yake inazidi kuzorota na kufafanua kuwa kati ya wajukuu hao sita ni yatima kwani wazazi wao walishafariki.
Bi Catherine akiwa na wajukuu zake
Social Plugin