Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHANDISI MIHAYO : WAANDISHI WA HABARI ACHENI KUCHEZA NA TASNIA YA HABARI.. USIANDIKE ANDIKE TU WALA KUTANGAZA TANGAZA TU

MENEJA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jiji la Tanga kushoto  ni na kulia ni Afisa Programu na Maendeleo ya Klabu, Utawala na Dawati la Jinsia kutoka (UTPC) Hilda kileo

Na Oscar Assenga, TANGA

MENEJA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini Mhandisi Francis Mihayo amewataka waandishi wa habari kuacha kucheza na tasnia ya habari kwa sababu watu wamepewa leseni na wakawapa kazi ya kuandika.

Mhandisi Mihayo aliyasema hayo wakati wa warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jiji la Tanga ambapo alisema kwa sababu watakapofanya kosa wao hawana haki ya kuwawajibisha (waandishi wa habari) bali ni chombo husika.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada ya sheria, kanuni za vyombo vya habari na maadili wakati wa uchaguzi ambapo alisema kuna mambo mengine hayako sawa ambayo wanayajua huku akieleza kwamba kuna baadhi ya waandishi wanahama kutoka vyombo vyengine na wengine hawasikikia hivyo wasifike huko.

“Kama wewe kazi yao ni kuandika andika tu na kutangaza tangaza tu usichanganye na mambo mengine tukiona kuna kasoro tutakwenda kwenye vyombo husika yale yote yanayofanywa yalio nje ya taaluma ya habari tunayaomba muachane nayo tumekuja kama rafiki tukigundua hicho kinaendelea na tutakifanyia kazi kupitia chombo husika”Alisema Mhandisi Mihayo.

Kuhusu wanaoendesha biashara za mitandao bila leseni aliwataka wale ambao hawana leseni wazihuishe haraka iwezekanavyo wasije wakaingia kwenye matatizo ikiwemo kuwataka kuwasiliana na mamlaka hiyo.

Katika hatua nyengine Meneja huyo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini aliwataka waandishi wa habari kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwenye chaguzi zijazo ikiwemo wa Serikali za Mitaa mwaka huu na ule mkuu wa mwakani 2025.

“Tatizo ni kwamba nyie waandishi wa habari mnauwezo wa kugombea na kuchukua nafasi lakini mnangoja wanachaguliwa viongoziz ambao hawawataki mnaanza kuwaandika kumbe nyie mnaweza kugombea na mkaongoza vizuri kule mwanza kuna madiwani waligombea na waandishi wa habari”Alisema Mhandisi Mihayo

Hata hivyo alitoa wito kwa waandishi wa habari mkoa huo kuwataka wawe kitu kimoja na asingependa kusikia migogoro ya waandishi wa habari bali washirikiane ikiwemo kuwataka kuacha kuandika stori ambazo haziko sawa.

Awali akizungumza katika warsha hiyo Afisa Programu na Maendeleo ya Klabu, Utawala na Dawati la Jinsia kutoka (UTPC) Hilda kileo aliishukuru mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kazi kubwa wanaiyoifanya na wanafurahi kuona wanaijali tasnia na kuendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari.

Alisema kwamba wanatambua waandishi ni kada muhimu nchini kwa sababu wana wajibu mkubwa wa kutengeneza wazo uwajibikaji pamoja na kusimamia maslahi ya umma kupitia kazi kuu tatu kuhabarisha, kuelimisha na kuburubisha.

“Tuna wajibu mkubwa nchini tujiangalie vizuri na kujitazma kama waandishi wa habari tuna kazi kubwa ya ya kusaidia kuleta uwazi, kusimamia maslahi ya umma ikiwemo kufanya kazi kwa ueledi “Alisema

Awali akizungumza katika semina hiyo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Lulu George aliwataka waandishi wa habari wahakikisha wanabadili na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Alisema wakati wanaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wamejiandaaje kwa sababu kuvunja shera kwa kukosa kutokujua sheria sio sababu ya kutokushtakiwa ikiwemo kuwataka waache kupuuza baadhi ya vitu.

“Tunaenda kwenye uchaguzi wao kama wana taaluma wakisema wategemee vyombo vya ulinzi ndio ilinde amani lakini waandishi wanapaswa kuilinda amani kwa kufuata maadili ya taaluma zetu, miiko ya taaluma kwa kuzingatia sheria za nchi kuziheshimu na kuacha kuvuka mipaka kwa sababu hakuna uhuru usio na mipaka”Alisema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George akizungumza wakati wa warsha hiyo katikati ni Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Fransic Mihayo na kulia ni Afisa Programu na Maendeleo ya Klabu, Utawala na Dawati la Jinsia kutoka (UTPC) Hilda kileo
Afisa Programu na Maendeleo ya Klabu, Utawala na Dawati la Jinsia kutoka (UTPC) Hilda kileo akieleza jambo wakati wa warsha hiyo

Na Oscar Assenga, TANGA

MENEJA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini Mhandisi Francis Mihayo amewataka waandishi wa habari kuacha kucheza na tasnia ya habari kwa sababu watu wamepewa leseni na wakawapa kazi ya kuandika.

Mhandisi Mihayo aliyasema hayo wakati wa warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jiji la Tanga ambapo alisema kwa sababu watakapofanya kosa wao hawana haki ya kuwawajibisha (waandishi wa habari) bali ni chombo husika.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada ya sheria, kanuni za vyombo vya habari na maadili wakati wa uchaguzi ambapo alisema kuna mambo mengine hayako sawa ambayo wanayajua huku akieleza kwamba kuna baadhi ya waandishi wanahama kutoka vyombo vyengine na wengine hawasikikia hivyo wasifike huko.

“Kama wewe kazi yao ni kuandika andika tu na kutangaza tangaza tu usichanganye na mambo mengine tukiona kuna kasoro tutakwenda kwenye vyombo husika yale yote yanayofanywa yalio nje ya taaluma ya habari tunayaomba muachane nayo tumekuja kama rafiki tukigundua hicho kinaendelea na tutakifanyia kazi kupitia chombo husika”Alisema Mhandisi Mihayo.

Kuhusu wanaoendesha biashara za mitandao bila leseni aliwataka wale ambao hawana leseni wazihuishe haraka iwezekanavyo wasije wakaingia kwenye matatizo ikiwemo kuwataka kuwasiliana na mamlaka hiyo.

Katika hatua nyengine Meneja huyo wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini aliwataka waandishi wa habari kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwenye chaguzi zijazo ikiwemo wa Serikali za Mitaa mwaka huu na ule mkuu wa mwakani 2025.

“Tatizo ni kwamba nyie waandishi wa habari mnauwezo wa kugombea na kuchukua nafasi lakini mnangoja wanachaguliwa viongoziz ambao hawawataki mnaanza kuwaandika kumbe nyie mnaweza kugombea na mkaongoza vizuri kule mwanza kuna madiwani waligombea na waandishi wa habari”Alisema Mhandisi Mihayo

Hata hivyo alitoa wito kwa waandishi wa habari mkoa huo kuwataka wawe kitu kimoja na asingependa kusikia migogoro ya waandishi wa habari bali washirikiane ikiwemo kuwataka kuacha kuandika stori ambazo haziko sawa.

Awali akizungumza katika warsha hiyo Afisa Programu na Maendeleo ya Klabu, Utawala na Dawati la Jinsia kutoka (UTPC) Hilda kileo aliishukuru mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kazi kubwa wanaiyoifanya na wanafurahi kuona wanaijali tasnia na kuendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari.

Alisema kwamba wanatambua waandishi ni kada muhimu nchini kwa sababu wana wajibu mkubwa wa kutengeneza wazo uwajibikaji pamoja na kusimamia maslahi ya umma kupitia kazi kuu tatu kuhabarisha, kuelimisha na kuburubisha.

“Tuna wajibu mkubwa nchini tujiangalie vizuri na kujitazma kama waandishi wa habari tuna kazi kubwa ya ya kusaidia kuleta uwazi, kusimamia maslahi ya umma ikiwemo kufanya kazi kwa ueledi “Alisema

Awali akizungumza katika semina hiyo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Lulu George aliwataka waandishi wa habari wahakikisha wanabadili na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Alisema wakati wanaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wamejiandaaje kwa sababu kuvunja shera kwa kukosa kutokujua sheria sio sababu ya kutokushtakiwa ikiwemo kuwataka waache kupuuza baadhi ya vitu.

“Tunaenda kwenye uchaguzi wao kama wana taaluma wakisema wategemee vyombo vya ulinzi ndio ilinde amani lakini waandishi wanapaswa kuilinda amani kwa kufuata maadili ya taaluma zetu, miiko ya taaluma kwa kuzingatia sheria za nchi kuziheshimu na kuacha kuvuka mipaka kwa sababu hakuna uhuru usio na mipaka”Alisema Mwenyekiti huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com