“Wizara itaendelea kutekeleza mradi wa mashamba makubwa ya Chinangali, Chunya, Singida na Ndogowe kwa kujenga mabwawa na kuchimba visima kwenye mashamba ya BBT jumla ya hekta 186,086. Vilevile, Wizara itaanza kutekeleza mradi wa BBT katika halmashauri 100 zitakazotenga maeneo yenye ukubwa wa hekta 200 kwa kila halmashauri na kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo hayo,” amesema Mhe. Bashe.
Programu hiyo inatekelezwa kupitia miradi mikuu minne ambayo ni kuwezesha upatikanaji wa ardhi ya kilimo na uanzishaji wa mashamba makubwa ya pamoja (Block farms) na umilikishaji wa ardhi, kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana na wanawake (BBT - Mitaji), kuimarisha Huduma za Ugani (BBT – Ugani) na kuwezesha upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo (BBT – Visima).