"Wizara ilipanga kutengeneza ajira 428,571 kwa mwaka 2023/2024 kupitia mipango na mikakati mbalimbali ikiwemo Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT). Ili kufikia malengo hayo, Wizara imeendelea kutekeleza Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora kwa vijana na wanawake yenye malengo ya kuongeza ajira zenye staha, kuongeza tija, kubakiza wakulima katika sekta (retention of farmers) na kupunguza umaskini.
Ninapenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, hadi Aprili, 2024 ajira 475,025 zimezalishwa katika Sekta ya kilimo sawa na asilimia 110 ya lengo la kuzalisha ajira 428,571 kwa mwaka 2023/2024.
Baadhi ya miradi na Programu iliyotekelezwa ni Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora kwa vijana na wanawake, miradi ya umwagiliaji na miundombinu ya uhifadhi na masoko." - Waziri wa Kilimo @HusseinBashe
Social Plugin