Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga akikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Muhalila
Na Mariam Kagenda_Kagera
Mdau wa michezo ambaye ni Mkurugenzi wa Mashindano ya Muhalila Cup Fortunas Muhalila amedhamini Mavazi ya Wanafunzi ambayo ni Traksuti 100 pamoja na Traksuti 13 za viongozi na walimu wa michezo katika mashindano ya UMITASHUMITA kwa shule za Msingi na UMISSETA kwa mwaka 2024 ili kuwawezesha Wanafunzi wa Wilaya ya Muleba kushiriki mashindano hayo kwa kujiamini.
Vifaa hivyo vya michezo vilikabidhiwa kwa niaba yake na Diwani wa kata ya Izigo Edwin Kaena kwa mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga ambaye alisema mdau huyo wa michezo amekuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha Wilaya hiyo inaendelea kupiga hatua kimichezo na kusema kuwa ataendelea kushiriki katika harakati mbalimbali za maendeleo ili kurudisha shukrani kwa jamii yake ambayo ilimfunza na kumlea.
Msemaji wa Muhalila Cup Omary Rwakaya amesema kuwa licha ya udhamini huo wa mashindano ya UMISETA na UMITASHUMITA pia waliwai kutoa mipira na vifaa vya michezo katika shule 70 za Wilaya ya Muleba ili kuendelea kukuza michezo na kuibua vipaji vya watoto.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dr Abel Nyamahanga alitoa shukrani kwa mdau huyo wa maendeleo kwa kuwa mdhamini na kuthamini michezo huku akiwahakikishia wadau na walimu wa michezo kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuendeleza michezo na mashindano hayo kwa ujumla huku akitoa onyo kwa walimu wanaowazuia Wanafunzi kushiriki michezo kwa kisingizio kuwa wanavipindi vingine .
Social Plugin