Na Mwandishi Wetu.
Ofisi ya waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeshiriki Maadhimisho ya kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 yaliyoanza tarehe 25 hadi 31Mei, 2024 mkoani Tanga yenye Kauli isemayo; "Elimu, Ujuzi, Ubunifu na Teknolojia kichocheo cha Maendeleo kwa Uchumi Shindani.
Maafisa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi hiyo wanaendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa nchini hususan kwa wanafunzi na watu mbalimbali wanaofika na kutembelea Banda la ofisi hiyo katika Maadhimisho hayo.
Aidha pamoja na hao wapo maafisa kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa pamoja wameendelea na uelimishaji umma kuhusu matumizi sahihi ya mbegu na faida za zao la mwani, katika Maadhimisho hayo Tanga.
Social Plugin