RAIS SAMIA ATAKA HAKI ZA RAIA KUFUATWA

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi katika ngazi zote kuendelea kusimamia haki za raia kama zilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa chachu ya mabadiliko chanya kifikra na kimtazamo.

Rais Samia amesema hayo jijini Dodoma katika hafla ya kupokea Ripoti ya Kamati ya Kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Kuangalia Jinai Nchini iliyofanyika Ikulu, Chamwino.

Aidha, Rais Samia ametoa rai kwa Viongozi kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Tume na kuhamasisha mabadiliko hayo kwa wananchi wanaowaongoza kwa lengo la kujenga upya ili kuimarisha utendaji unaozingatia misingi ya utawala bora.

Vile vile, Rais Samia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kutekeleza mamlaka yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na mipaka ya mamlaka hayo.



Rais Samia pia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inailinda na kuimarisha misingi ya utu, usawa, haki na uongozi bora hapa nchini.

"Ili kujenga uelewa wa pamoja wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai, Rais Samia amewataka Makatibu Wakuu Viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuandaa warsha kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, " Amesema  Rais Samia.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post