"Wakati wa utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2023/2024 Serikali ilikabiliwa na tatizo la upungufu wa sukari ambao ulitokana na mvua za EL-Nino na tabia za wafanyabiashara kutengeneza uhaba wa sukari (artificial scarcity) kwa kutokuingiza sukari ya kuziba pengo (gap sugar) kulingana na vibali vya uagizaji walivyopatiwa na hivyo kupandisha bei ya sukari.
Hali hiyo ilisababisha kupanda kwa bei ambapo hadi tarehe 22 Januari, 2024 wastani wa bei ya jumla kwa wazalishaji wakubwa nchini ilikuwa ni kati ya Shilingi 3,800 na 4,000, wauzaji wa jumla kati ya Shilingi 4,500 na 5,000 na bei ya rejareja kati ya Shilingi 6,000 na 10,000 kwa kilo moja katika maeneo mengi, hali ambayo ilikuwa inahatarisha usalama wa nchi na uchumi wetu.
Serikali itaendelea kuvilinda viwanda vya ndani na kuwalinda wakulima wa miwa lakini ulinzi huo hautakuwa kwa gharama ya kuwatesa Watanzania milioni 61.
Social Plugin