SERIKALI HAITAVUMILIA UPANDISHWAJI WA BEI YA SUKARI KIHOLELA

 

"Wakati wa utekelezaji wa  Bajeti ya Mwaka 2023/2024 Serikali ilikabiliwa na tatizo la upungufu wa sukari  ambao ulitokana na mvua  za EL-Nino na tabia za wafanyabiashara kutengeneza uhaba wa sukari (artificial scarcity) kwa kutokuingiza  sukari ya kuziba pengo (gap sugar) kulingana na vibali vya uagizaji walivyopatiwa na hivyo kupandisha bei ya  sukari. 


Aidha, kiasi cha sukari walichoingiza nchini  hawakukisambaza kama ilivyokusudiwa ili kutatua  changamoto ya upatikanaji wa sukari. 


Hali hiyo ilisababisha  kupanda kwa bei ambapo hadi tarehe 22 Januari, 2024  wastani wa bei ya jumla kwa wazalishaji wakubwa  nchini ilikuwa ni kati ya Shilingi 3,800 na 4,000,  wauzaji wa jumla kati ya Shilingi 4,500 na 5,000 na bei  ya rejareja kati ya Shilingi 6,000 na 10,000 kwa kilo moja katika maeneo mengi, hali ambayo ilikuwa inahatarisha usalama wa nchi na uchumi wetu.


Serikali itaendelea kuvilinda viwanda vya ndani na kuwalinda wakulima wa miwa lakini ulinzi huo hautakuwa kwa gharama ya kuwatesa Watanzania milioni 61.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم