SERIKALI YATAKA TATHMINI ITUMIKE KUONGEZA UFANISI WA SHUGHULI ZAKE

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati akifungua kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma tarehe 14 Mei, 2024.

Mkurugenzi Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu akitambulisha wajumbe wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Rahma Mahfaudh akifafanua jambo wakati wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma.


Na. Mwandishi wetu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza itumike katika kuongeza Ufanisi na Utendaji wa Shughuli za Serikali ili kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya kwa Maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kilichofanyika tarehe 14 Mei, 2024  katika Ukumbi wa Nssf Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajumbe wa kikao hicho kutumia Makongamano hayo kwa lengo la kuonesha fursa zaidi ya kile kinachotarajiwa katika kuwavutia wawekezji nchini.

“Yatumieni makongamano haya kwa tija na mshirikishe wadau kwa lengo la kuendeleza ushirikiano na kuchochoea wawekezaji nchini, hivyo Makongamano haya yahusishe sekta za kiuchumi ikiwemo za utalii, uwekezaji pamoja na masuala ya sanaa na utamaduni ili kuchagiza mazingira bora ya biashara na uwekezaji,"  alisisiza Dkt. Yonazi

Kongamano hilo la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2024

Baadhi ya Washiriki wa kikao cha pili cha Maandalizi ya Kongamano la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza wakifuatilia kikao hicho.



























Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post