Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025 amesema kuwa uzalishaji wa chakula kwa msimu wa kilimo wa 2022/2023 ulitosheleza mahitaji ya chakula ya tani 16,390,404 kwa mwaka 2023/2024 na kuwepo kwa ziada ya tani 4,011,611.
Amesema kutokana na hali hiyo, Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 124 ikilinganishwa na utoshelevu wa asilimia 114 mwaka 2022/2023. Aidha, utoshelevu wa chakula unatarajiwa kufikia asilimia 130 ifikapo mwaka 2025
Social Plugin