UKARABATI WA MV. MAGOGONI KUKAMILIKA DISEMBA 2024

 

Na Dotto Kwilasa, Bungeni-Dodoma

Ukarabati wa Kivuko cha Mv. Magogoni unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwezi Desemba, 2024 na kurejeshwa Nchini ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 30 Mei 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile aliyeuliza ni lini matengenezo ya Pantoni ya Mv. Magogoni iliyopo nje ya Nchi yatakamilika na kurejeshwa nchini ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Itaumbukwa kuwa Mwezi Februari 2023 Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ilisaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.5.

Lengo la ukarabati huo wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini, kuharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post