Baada ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwasilisha Bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2024/25, wanafunzi wa vyuo mbalimbali wameibuka na kuunga mkono huku wakipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika.
Dankan Esao, mwananfunzi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ameonyesha kufurahishwa na msisitizo wa Serikali katika kukuza ujuzi wa uandishi, kuhamasisha tabia ya usomaji na kuongeza machapisho katika maktaba nchini.
"Tunaishukuru Serikali kwa kutambua tafiti na waandishi tofauti tofauti kwa kuwpaa tuzo na kuchochea karama za usomaji ili nchi iwe na utamaduni kwa kusoma, hatua hii pia itaboresha mahusiano mazuri kati ya jamii na maktaba kwani Watanzania wengu hatukuwa na utaratibu huo hapo awali," amesema Dankan.
Social Plugin