Hayo yamesemwa na Mhe. Hussein Bashe wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo leo Tarehe 02.05/2024 Jijini Dodoma ambapo amesema ongezeko hilo limechangiwa na uzalishaji wa korosho ambao umefikia tani 254,500 ikilinganishwa na tani 189,113.79 mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la asilimia 63.6 ya lengo la kuzalisha tani 400,000 mwaka 2023/2024.
Aidha Mhe. Bashe amesema uzalishaji wa pamba umefikia tani 282,510 ikilinganishwa na tani 174,486 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 80.7 ya lengo la kuzalisha tani 350,000 mwaka 2023/2024; na uzalishaji wa sukari umefikia tani 392,724 .
Katika uzalishaji wa zao la kahawa amesema uuzalishaji umefikia tani 66,071.8 ikilinganishwa na tani 82,000 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 77.7 ya lengo la kuzalisha tani 85,000; uzalishaji wa pareto ambao umefikia tani 4,238 ikilinganishwa na tani 3,150 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 121.08 ya lengo la kuzalisha tani 3,500; uzalishaji wa mkonge ambao umefikia tani 56,732.7 ikilinganishwa na tani 48,359.49 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 94.55 ya lengo la kuzalisha tani 60,000.
Pia Mhe. Bashe amesema uzalishaji wa chai ambao umefikia tani 13,525 ikilinganishwa na tani 26,753 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 45 ya lengo la kuzalisha tani 30,000.
Social Plugin