Gwaride la Heshima la Vijana wa kujitolea likipita mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli (hayupo pichani) kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,hafla iliyofanyika Mkoani Kigoma.
MKUU wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli,akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,hafla iliyofanyika Mkoani Kigoma.
MKUU wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,hafla iliyofanyika Mkoani Kigoma.
Kamanda Brigedi 202,Brigedia Jenerali Gabriel Kwiligwa,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,Mkoani Kigoma.
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,Mkoani Kigoma.
Kamanda Kikosi cha 821 KJ Bulombora, Luteni Kanali Juma Hongo,akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,Mkoani Kigoma.
Baadhi ya Wananchi wakifatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,Mkoani Kigoma.
Vijana wa JKT wakionyesho ufundi wao kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora,Mkoani Kigoma.
Na.Alex Sonna-KIGOMA
MKUU wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli amewataka vijana waliopata mafunzo ya awali Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yaliyo kinyume na mila na utamaduni wa Watanzania.
Mhe.Kalli ameyasema hayo Mkoani Kigoma wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea 'Operesheni ya Miaka 60 ya JKT', katika kikosi cha Jeshi cha 821, Bulombora.
Mhe.Kalli,amewaonya juu ya matumizi ya mitandao ya jamii yanayotokana na ukuaji wa teknolojia ambayo yamemfanya kila Mtanzania kutamani kutumia simu janja ambazo zimekuwa na mambo mengi kiasi cha mtu kufahamu kila kinachofanyika duniani kupitia mitandao ya kijamii.
“Vijana wengi wamekuwa hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, hivyo basi hutazama mambo ambayo ni kinyume kabisa na tamaduni zetu za kiafrika. Ninawaomba sana msiingie huko kwenye mitego isiyo yenu, hakikisheni mnalilinda Taifa lenu,”amesema Mhe.Kalli
Aidha amewataka kuhakikisha wanalinda Taifa, wanasimamia miongozo, uadilifu na maelekezo ya kila siku ili nchi iendelee kuwa salama.
Pia amesema kuwa Serikali ilitunga Sheria ya Kudhibiti Maudhui Mtandaoni ambapo watakapopatikana na maudhui ambayo ni kinyume na mila na utamaduni, hatua kali za sheria zitacjhukuliwa dhidi yao.
“Natumia fursa hii kuwaasa kuwa hatutakuwa na wasaa mwingine tutakapokuta wewe umeingia kwenye makundi yasiyofaa ambayo siyo yale uliofundishwa hapa (jeshini) ukaingia katika mitandao ya hatakuwa na saa nyingine ya kutoa wasia wakati watakapofanya mambo ya hovyo, bali watawachukulia hatua za kisheria mara moja,”amesema. Aidha, amewataka kusimamia nchi yao kuwa wazalendo, waadilifu na kutokubali nchi yao ikalindwa na watu wengine na badala yake kulinda wenyewe kwa utii waliofundishwa lakini wakisimamia kiapo chao na miongozo na maelekezo ya Amiri Jeshi Mkuu Dk Samia Suluhu Hassan.
Mhe.Kalli ameipongeza Serikali chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha ufanyikaji wa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa ustawi wa Vijana wetu na Taifa kwa ujumla. "Nipende kulishukuru Jeshi la Kujenga Taifa na Watendaji wote chini ya uongozi Shupavu wa Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele kwa kusimamia kwa weledi mkubwa malezi ya vijana wetu na hatimaye kufikia viwango bora."
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji mawazo ya muasisi wa Taifa, Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere katika uanzishwaji wa JKT.
”Naamini kuwa mafunzo haya mliyoyapata mmekuwa tayari kulitumikia na kulilinda taifa letu popote mtakapokuwa kwani mmefahamu dhana ya uzalendo, umoja, mshikamano, ukakamavu na kujiami, mnapaswa kutumia elimu hii katika kutatua changamoto mbalimbali pasipo kuvunja sheria na taratibu za nchi. Hivyo nendeni mkaishi kiapo chenu.”amesema Brigedia Jenerali Mabena
Aidha Brigedia Jenerali Mabena amewataka vijana hao kutunza afya zao kwani ndio msingi na mtaji wao mkubwa na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, ulevi, utumiaji wa dawa za kulevya, ulaji wa vyakula au utumiaji wa vinywaji vyenye kuhatarisha afya zao.
Awali, Kamanda Kikosi cha 821 KJ Bulombora, Luteni Kanali Juma Hongo, amesema mafunzo ya vijana wa kijitolea Operesheni miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa yalianza Desemba 2023 na kufanyika kwa majuma 16 mfululizo ambapo vijana wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo mbinu za kivita, ujanja wa porini, usomaji wa ramani, usalama na utambuzi kukabliana na majanga na matumizi ya silaha ndogondogo, kazi za mikono na uzalishaji mali kwa vitendo.
”Lengo likiwa ni kukuza moyo wakizalendo, kuwajengea ukakamavu, ujasiri, uwezo wa kutumia muda vizuri kwa kufanyakazi na pia wajitambue kuwa wao ni sehemu ya jamii ya watanzania wanaopaswa kupata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.”amesema Luteni Kanali Hongo
Social Plugin