Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), amesema wizara itapima afya ya udongo katika maeneo mapya ya uwekezaji yatakayoainishwa katika mikoa ya Simiyu, Mara, Geita, Tabora, Songwe na Tanga kwa kuhusisha maeneo kwa ajili ya vijana na wanawake kupitia Programu ya BBT; kuendelea kutoa huduma ya kupima afya ya udongo kwa wakulima wakubwa na wadogo bure kwa kutumia vifaa vya kupima afya ya udongo vilivyosambazwa katika halmashauri.
Mhe. Bashe amesema hayo wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025, leo Alhamisi Mei 2, na kuongeza kuwa wizara yake itabuni na kuhamasisha matumizi ya teknolojia sahihi za utunzaji wa maji na udongo mashambani ili kulinda vyanzo vya maji kwa ajili ya umwagiliaji katika mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya.
Vilevile, Wizara itanunua mobile soil laboratory van kwa ajili ya kupima afya ya udongo.