Ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike pamoja na uongezaji vifaa katika vyuo vya ufundi ni miongoni mwa mambo yaliyowagusa wanafunzi wa elimu ya juu ambapo wameishukuru Serikali kwa jitihada inayoendelea kuzifanya kukuza sekta ya elimu.
John Chifuka, mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) akizungumza baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2024/25 ameonekana kufurahishwa na hatua hiyo ya Serikali.
"Kuongezwa kwa vifaa na vitendea kazi inasaidia wanafunzi katika vyuo vya ufundi kufanya shughuli zao na masomo yao kwa vitendo zaidi, lakini pia kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi kunachochea wanafunzi kujinufaisha zaidi," amesema Chifuka