WAZIRI MKUU AVUTIWA NA UBUNIFU UDOM


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, akipata maelezo kutoka kwa mbunifu wa vifungashio kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Bw. Mohammed Amini, Mkufunzi Msaidizi kutoka Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati.

.......

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amevutiwa na ubunifu uliofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.

Akizungumza wakati alipotembelea Banda la UDOM katika Kilele cha Maadhimisho hayo Ijumaa tarehe 31 Mei, 2024, Mhe. Majaliwa amekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuweza kubuni vifungashio mbadala ambavyo ni rafiki kwa Mazingira, na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Aidha, ametoa wito kwa UDOM kuendelea kufanya tafiti na kuja na bunifu nyingi za kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, likiwemo suala la vijana kujiajiri. Naye, mbunifu wa vifungashio hivyo kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma ambaye ni Mkufunzi Msaidizi Bw. Mohammed Amini, kutoka Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati amesema vifungashio hivyo vinatengenezwa kwa malighafi taka na zao la mwani na hivyo gharama za kuzalisha ni ndogo kiasi cha kila mwananchi kuzimudu, na pia ni bidhaa rafiki katika kutunza mazingira.

Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yalianza tarehe 25 Mei na kufungwa tarehe 31 Mei 2024, yakiwa yamefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Tanga, yakihusisha wadau wote wa Elimu nchini vikiwemo Vyuo Vikuu, Vyuo vya Kati, Taasisi na Mashirika ya Elimu.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, akiwasili kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal Tanga, yanakofanyika maadhimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka (mwenye suti kulia) akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dodoma kwenye kilele ya Wiki ya Elimu Tanga.


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, akipata maelezo kutoka kwa mbunifu wa vifungashio kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Bw. Mohammed Amini, Mkufunzi Msaidizi kutoka Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, akieleza jambo wakati wa akiwa kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Elimu yaliyofanyika mkoani Tanga.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, akikagua mfuko uliotengenezwa kwa bidhaa taka na zao la Mwani, alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma.


Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu Mkoani Tanga. Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na maonesho ya Elimu, Ubunifu na Teknolojia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post