Akizungumza Jijin Dar es saalaam juzi wakati alipotembelea Ofisi za JamiiForums,
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye amesema
Serikali inaamini katika uhuru wa Watu kujifanyia maamuzi wenyewe.
Amesema mazungumzo hayo yatahusisha kuweka “mechanism” ya kushirikiana ili kuhakikisha taarifa sahihi zinafanyiwa kazi ndani ya muda mfupi na Wananchi kujulishwa
Amesema “Ni rahisi mtu kuja na taarifa ya uongo na kupoteza mwelekeo kwa Wananchi zaidi ya milioni 60.
“Sisi (Wizara) tutakuwa mabalozi wa JamiiForums ili mfanye kazi na Wadau mbalimbali kwa kuwa wote tuna lengo moja,amesema Nape
Amesema wakati mwingine Wanasiasa au viongozi hudhani
wanajua zaidi kuliko Wananchi lakini ukweli ni kuwa Wananchi wanajua
wanachokitaka, wanatakiwa tu kupewa taarifa sahihi.
Katika hatua nyingine amesema “Nimefurahi kuja JamiiForums sikuwa najua kama mna ukubwa wa kiasi hiki, kwa mambo mnayoyafanya ninyi ni Wadau wangu wa muhimu sana, mnafanya kazi kubwa, mna historia yetu ambayo ni nzuri na vizuri mkaendelea kuitunza.”
Ameongeza “Moja kati ya malengo ya Wizara ni kuhakikisha Jamii inakuwa na taarifa sahihi kwa sababu tunaamini ikiwa na taarifa sahihi za kutosha itakuwa chachu ya wao kujiletea maendeleo na kutatua matatizo yao ya msingi ikiwemo Afya, Elimu na mengine mengi.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo, amesema wana mpango wa kutengeneza simu janja Zaidi ya millioni 10 kwa miezi tisa ijayo ambayo itaenda kuwasaidia wananchi walio vijijini hususani vijana na wanawake zinazotarajiwa kuuzwa kwa bei ya chini ya elfu 50.
Social Plugin