TEKNOLOJIA MPYA YA BAJAJI NA PIKIPIKI ZINAZOTUMIA MFUMO WA UMEME KUANZA KAZI JIJINI TANGA


Na Hadija Bagasha Tanga,

Vijana 75 kutoka chuo cha mafunzo ya ufundi stadi VETA na SIDO jijjni Tanga wamepatiwa mafunzo ya namna ya utumiaji wa teknolojia mpya ya vyombo vya moto ikiwemo bajaji na pikipiki zinazotumia mfumo wa umeme jijini Tanga.

Vijana hao ambao 40 wametokea katika Chuo cha mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) Mkoani Tanga na wengine 35 kutoka SIDO pamoja na katika baadhi ya gereji jijini humo, wamepatiwa mafunzo hayo June 25 mwaka huu juu ya namna ya matumizi ya bajaji hizo yaliyoandaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Open Innovation chini ya kampuni ya ROBOTECH LABS.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, 0fisa Mradi huo Abdulwahab Issa  amesema vijana hao wamejifunza na kuona namna bajaji hizo zinavyofungwa pindi zinapotoka viwandani lakini pia wameweza kujionea mifumo ya umeme na mota vinavyofanya kazi pamoja na kutengeneza na kutumia vyombo hivyo. 

"Lengo kubwa ni vijana kuweza kupata 
aware  na kujionea kwa macho namna vyombo hivi vinavyofanya kazi lakini pia watakavyokwenda kuvisimamia wakati wa kufanya kazi katika kuokoa na kujiingizia kipato katika shuhuli zao za kila siku, 

"Bajaji hii ina uwezo wa kutembea kilomita 80 hadi 100, kwa chaji iliyojaa kwa asilimia 100 kwa umeme wa sh elfu 3, hapo inaweza ikatuonesha kwamba ni namna gani unaweza kwenda ukaokoa kipato chako cha matumizi katika ununuaji wa mafuta" amesema. 

Haji amesema sambamba na hayo,  wamelenga kutoa mafunzo kwa vijana hao ili kupata mafundi watakaoweza kujua kujua jinsi ya uendeshaji,  uundaji pamoja na ueekebishaji wa vyombo hivyo lakini pia wasambazaji wa vyombo hivyo kama bidahaa zitakapotoka viwandani. 

"Wito wangu wa vijana wa Mkoa wa Tanga,  waendelee kujitokeza pale fursa hizi zitakapotokea, hizi fursa ni adimu na ni mara chache zinapokuwa zintolewa bure kwasababu hakuna garama zozote wanazolipia, waje wajionee, wajifunze ili waje waweze kuwa mafundi, madereva ma wasambazaji wa huduma za bidhaa hizi za bajaji" ametoa wito. 

Hata hivyo amebainisha kwamba kikubwa zaidi ni katika jitihada za utynzaji wa mazingira kuhakikisha nchi inatoka kwenye matumizi ya nishati chafu na kuelekea kwenye matumizi ya nishati safi hivyo kulenga kuanzabkutumia tekinolojia ya nishati ya umemevna kuachana na matumizi ya mafuta. 

Baadhi ya walioshiriki mafunzo hayo  wameelezwa kwamba mafunzo hayo yamewapa mwangaza mkubwa na kuona ni jinsi gani tekinolojia hiyo inaenda kuwafanikishia katika kipato chao pindi watakapotumia bajaji hizo.  

Kwa upande wake Afisa vijana kutoka Halmashauri ya jiji la Tanga Fadhili Secha amesema teknolojia hiyo inakwenda kuwarahisishia vijana matumizi makubwa ya nishati ya mafuta ya petrol lakini pia ni tejnolojia hiyo inakwenda kuwasaidia kupata faida wanapoendesha shughuli zao za usafirishaji. 

Mwenyekiti wa waendesha bajaji Mkoa wa Tanga Rahimu Makange amesema "Kwa upande wangu nimeona hii ni fursa kubwa sana na mafunzo haya yananifanya nijione kuwa ni Injinia mkubwa sana kwa sasa, na hizi bajaji nimeona zinarahisisha mambo mengi.

Naye Halfani Rashidi dereva wa bajaji jijini Tanga amesema, bajaji hii ya umeme tayari nimeshaanza kuitumia na manufaa yake ni makubwa,  kwasababu nikiwa natumia bajaji ya kawaida nilikuwa natumia zaidi ya sh elfu 15 kwa siku lakini hii natumia umeme wa sh elfu 3 kwa siku, ni rahisi sana" ameeleza

"Hazina garama kubwa, ni suala la kuhakikisha tu hukosi luku, lakini suala la kuingia sheli kupanga foleni kutafuta petroli au dizeli hakuna, na kwamba unapokuwa na umeme wa sh elfu 3 unaweza ukasafiri kutoka Tanga hadi Korogwe,  lakini ni petroli matumizi yangekuwa makubwa sana". 

Teknolojia mpya ya matumizi ya bajaji za mfumo wa umeme inatajwa kwenda kuaongezea kipato vijana wengi lakini pia inakwenda kuwaondolea gharama za nishati ya mafuta watumiaji wa vyombo hivyo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post