Na Hadija Bagasha Tanga
Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 379.5 kwa ajili ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wa awali kwenye jiji la Tanga kupitia mradi wa BOOST kwenye shule tano za msingi jijini humo.
Afisa elimu ya msingi na timu yake ya utekelezaji wa mradi huo amefanya mkutano kwenye shule ya msingi Mwakidila vinapojengwa vyumba viwili na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Shomari Bane amesema ujenzi wa vyumba hivyo utaenda sambamba na matundu sita ya vyoo, uzio , michezo ya watoto na shamani, vyote vikiwa na gharama ya Tsh milioni 69,100,000.00, huku akisema mradi huo utaleta tija kubwa kwenye sekta ya elimu.
Shele nyingine alizozitaja zitakazonufaika na mpango huo Kasera pamoja na shule shikizi ambayo imepata kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na shiling milioni 12.6 kwa ajili ya kujenga matundu sita ya vyoo,
Alisema shule ya msingi Mwakidila pia imepatiwa sh milioni 69.1 kujenga madarasa mawili pamoja na matundu 6 ya vyoo, matundu matatu ya wavulana na matatu ya wasichana.
"Lakini kama haitoshi nimewaomba sana wananchi kutumia nguvu zao kujitolea na michango yao kwa ajili ya kujenga ofisi ya walimu kwa sababu kuna watoto hawa wadogo wa elimu ya awali, hivyo wanapokuwa na ofisi jirani na walimu wao itapendeza zaidi kiusalama" amesema.
Amefafanua kwamba shule za msingi Majengo na Shaban Robbert kila moja ilipatiwa sh milioni 75 kwa ujenzi wa madarasa matatu pamoja sh milion 12.6 kwa ajili ya matundu 6 ya vyoo.
Hata hivyo mpango wa kujenga madarasa kwenye shule hizo, ulibadilishwa na zimepekwa kwenye shule zingine za msingi Ziwani na Kange, kwa kuwa, Shaban Robart na majengo upo mpango wa kujengwa ghorofa.
"Mradi huu unatekelezwa ndani ya miaka sita, kuanzia mwaka 2021 hadi 2027 na mradi hu tunaukabidhi kwa uongozi wa kata katika shule husika kwakuwa wao ndiyo watakaosimamia mradi huu", amefafanua Bane.
Baadhi ya wananchi wameelezea furaha yao kufuatia mradi na kusema itawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuweza kukaa madarasanu kwa nafasi kwani vyumba vya madarasa ju vichache ikilinganishwa na wanafunzi waliopo.
Mwenyrkiti wa mtaa wa Mwakidila B, Athumaji Mbulinyingi amesema mradi huo kwa upande wao ni kama upendeleo mkubwa wanaishukuru sana serikali ya awamu ya sita kwani kil9 chao kikubwailikuwa ni kero kubwa sana kwakuwa watoto walikuwa na msongamano mkubwa.
"Tunaishukutu sana serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendeleo huu, tuna imani kubwa sana na mradi huu na mimi kama mwenyekiti wa mtaa nitausimamia nikishirikiana na wananchi wangu, nina imani utafanyika na hakutakuwa na dosari yoyote na utafikia hatma pasi na malumbano wala mgogoro wa aina yoyote", amesema .