NTOBI : CHADEMA HAINA MGOGORO, MBOWE NA LISSU NI KITU KIMOJA "SUNGUSUNGU MKOME KUNYANYASA WATU"

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi ameeleza kuwa hakuna mgogoro baina ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu.

Ntobi ameyasema hayo Juni 15,2024 kwenye mkutano wake wa hadhara katika kata ya Maganzo jimbo la Kishapu ambapo amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa na sintofahamu na kudhani kuwa kuna mgogoro ndani ya CHADEMA baina ya Mwenyekiti Mbowe pamoja na Lissu.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi amewatoa hofu watanzania kuwa hakuna mgogoro ndani ya CHADEMA huku akihimiza kuendelea kukiunga mkono chama hicho katika utetezi wa haki za wananchi.

“Chama chetu cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika Tanzania hii hakina mgogoro wowote, hatuna mgogoro baini ya Mhe. Lissu wala hakuna mgogoro baini ya Mhe. Lissu na Mhe. Mbowe wote hawa ni majembe ni kitu kimoja Chama chetu kuna mtu tu mmoja hakushinda uchaguzi mmoja akaingiza mgogoro wa kwake binafsi, jambo hilo nimekuwa naulizwa nimeona ni vema niwaambie na watu wa Maganzo maana CCM wamechukua kama Propaganda ya kusema CHADEMA imesambaa CHADEMA itabomoka hiki chama hakitabomoka kwa sababu CHADEMA ni mpango wa Mungu”,amesema Ntobi.

Katika hatua nyingine Ntobi amemsisitiza mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringa Macha kushughulikia changamoto za jeshi la jadi Sungusungu kuwa baadhi ya watu katika jeshi hilo hutajwa kukamata na kutishia wananchi.

“Nimtumie salamu mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha nataka nimwambie tabia ya Sungusungu iliyokithiri katika jimbo la Kishapu kukamata, kutishia watu kukusanya michango hii tabia tutamshtaki yeye na hao Sungusungu wake”.

“Sungusungu hawapo kwenye sheria yoyote ya nchi ni wanafanya kazi kihuni tu na wamelelewa kihuni na Chama Cha Mapinduzi kuwatisha watu wanaotetea haki hakuna sheria yoyote ya Sungusungu katika taifa hili na ninyi watu wa Maganzo na vijiji vingine kakataeni, nimeambiwa kuwa baadhi ya Sungusungu walikwisha kupelekwa Mahakamani, sasa mimi namtumia salamu mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Shinyanga jambo hili halipo Kishapu tu lipo Solwa, lipo Ushetu, lipo Shinyanga mjini kwenye kata ya Kolandoto hawa Sungusungu wakome kabisa kuwanyanyasa wananchi”, amesema Ntobi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi ameitaka serikali kushusha bei za mafuta ya Petroli ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini.

Pia Ntobi amewahimiza wananchi wa jimbo la Kishapu na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la makazi pamoja na daftari la kudumu la wapiga kura ili kushiriki vyema katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu Mwaka 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara katika kata ya Maganzo jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara katika kata ya Maganzo jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga
Wananchi wa kata ya Maganzo jimbo la Kishapu wakiwa katika mkutano wa hadhara ambao umeandaliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi.

Mkutano wa hadhara ukiendelea katika kata ya Maganzo jimbo la Kishapu.

CHANZO - MISALABA BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post