Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wamefanya ziara ya kutembelea Kituo cha kupokelea gesi asilia-Kinyerezi leo Jumatatu Juni 10, 2024 kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na GASCO ikiwemo shughuli za uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya gesi asilia, shughuli za ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia pamoja na shughuli za ulinzi na usalama wa miundombinu ya gesi asilia.
Muonekano wa sehemu ya miundombinu ya gesi asilia katika kituo cha kupokelea gesi-Kinyerezi
Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO Mhandisi Baltazar Mrosso akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Bodi ya TPDC.
# TPDC TUNAWEZESHA
Social Plugin