Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC wamepongeza jitihadaa zinazofanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kuwajengea uwezo wafanyakazi wanaoendesha mitambo ya kuchakata gesi asilia Songosongo na Madimba ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi, hii imewezesha wafanyakazi hao kuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha mitambo hiyo.
Akiongea katika ziara hiyo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mjiolojia Bwana Salavatory Ntomola alisema “Ni jambo la kujivunia kwa TPDC na Nchi kuona mitambo hii ikiendeshwa na watanzania kwa asiliamia mia moja’’.
#TunawezeshaMaisha
Social Plugin