Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NG'WANA KANG'WA MSANII WA KWANZA TANZANIA - BALOZI WA BIA ZA GOLDBERG NA HANSON'S LITE


Msanii maarufu wa Nyimbo za Asili Ng'wana Kang'wa amekuwa Msanii wa Kwanza Tanzania anayefanya Muziki wa Asili kupewa Ubalozi wa Kutangaza Vinywaji Vipya (Bia) maarufu Goldberg na Hanson's Lite zinazotengenezwa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) Shinyanga ambayo pia  inatengeneza vinywaji vya Diamond Rock na Hanson's Choice!

Ng'wana Kang'wa 'Ambassador wa Goldberg na Hanson's Lite beer' Kutoka kampuni East African Spirits' pia anakuwa Msanii wa Kwanza nchini Tanzania kupewa shavu la kutangaza bia za  Goldberg na Hanson's Lite ambazo zimepokelewa kwa kishindo na wadau zikiwa ni bia za kipekee zenye ladha ya kipekee sana!! 




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com