Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Ndg Jumanne Wambura Wagana amekabidhi madawati 40 kwa shule ya msingi Kasebuzi Mkoani Kigoma ambapo madawati hayo yamepokelewa na mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mh. Aggrey John Magwaza ikiwa ni mwendelezo wa benki hiyo ya CRDB katika kutekeleza sera yake ya uwekezaji kwa jamii na kampeni ya KETI JIFUNZE inayolenga kupunguza uhaba wa madawati mashuleni.
Akipokea Madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mh. Aggrey John Magwaza ameishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo mkubwa na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano mkubwa zaidi kibiashara huku akiwasisitiza wazazi walimu na wanafunzi kuendelea kutumia Huduma za CRDB na kuwaasa wadau wengine kuiga mfano huo na kurudisha kwa jamii.
Social Plugin