Mwanamke wa miaka 80 amezua tafrani kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuripotiwa kuolewa na mwanaume mwenye umri wa miaka 22.
Katika video ambayo iliyopepea TikTok, wanandoa hao wamenaswa kwenye sherehe ya harusi yao ya kitamaduni, huku kijana huyo akimvisha pete kidoleni mpenziwe.
Tukio hilo linasemekana lilitokea Tema Newtown huko Accra.
Marafiki, familia na wapendwa wachache walikuwepo kushuhudia hafla hiyo.
Wanandoa hao wenye furaha wote walikuwa wakitabasamu, na kama wengi wanasema, umri ni idadi tu kwa wanamtandao.
Hii si mara ya kwanza kwa wanandoa walio na tofauti kubwa ya umri kufunga pingu za maisha na hadithi yao kupepea mitandaoni.
Wanamtandao waliguswa na ajuza mwenye umri wa miaka 80 kuolewa na kijana mchanga kiasi hicho.
Wanamtandao walioona video hiyo walionyesha maoni tofauti; baadhi waliwapongeza wanandoa hao, huku wengine wakimtuhumu kijana huyo kumuoa mwanamke huyo kwa utajiri wake.
Jamani sidhani kama ni ukweli." @STANLEY aliandika:
"Hakuna ubaya wowote hapa sasa." @Abieku aliandika:
"Unastahili kupendwa pia." @Graceayesu aliandika:
"Labda ni wenzi wa roho." @ireneeedeh aliandika:
"Awaii mama mkubwa." @Aba Aggrey aliandika:
"Eeeoiii, nini kinaendelea?" @Jay_y alishangaa:
"Mmmmm." @Euniceselormey266 aliandika:
"Hmmmmmm." @Rich hunty aliandika:
" Na kwa hivyo ni chaguo gani." @Sister Adwoa aliandika:
"Paspoti ya Marekani anaa." @Queen Essie aliandika:
"Huyu jamaa naye. Huyu ni nyanyake jamani."
TAZAMA VIDEO YENYEWE HAPA
@one_minute_news_ ♬ original sound - One Minute News
Social Plugin